Utumwa

Haya ndio aina ya mabadiliko katika jumuiya yanayoleta maendeleo katika jamii nahatimae kuleta mabadiliko ya uzalishaji mali wa aina mpya. Haya ndio aina yamabadiliko ya uzalishaji mali ambayo hufanya mtindo wa uzalishaji mali fulani kamavile wa utawala kubadilika. Njama mpya hizi huwa kwa desturi ni alama yamaendeleo ikifananishwa na nyenendo zilizo kwisha pita. Utumwa kwa vile ulikuwa uzalishaji mali kongwe na zorota ulibidi ubadilike napahala pake kuchukuliwa na uzalishaji mali wa "Kibwanyenye/Kimwinyi". Uzalishaji huu wa mali ulimfanya mtumwa kuwa huru kwa kiwili wili, lakini si kiuchumi walakifikra, kwani uhuru aliyoupata ulikuwa uhuru wenye vigezo na vikwazo fulani.Mtumwa hapo akawa mtumishi wa rasilmali na mfumo mpya wa kisiasa, akiwa nakiwili wili chake tu huru wakati nguvu zake na akili yake zikiwa si mali yake,yaani akiweza kuchagua tajiri/bwanyenye /bwana gani atamtumikia kwa malipoasiyooweza kuyakatia uamuzi, na mara nyengine hata kutoweza kuchagua muajiriwake. Mtu huyu baada ya kupata uhuru wake ilimbidi ijipatie makaazi, chakula,nguo, matibabu, ulinzi n.k. yeye mwenyewe, wakati mambo hayo huko nyumayakihudumiwa na yule aliye mmiliki. Kwa mara nyingi kiwanja chakujengea nyumba yenyewe au upangishaji wake, ulitokana na muajiri wake, mara nyingiakiwa yule yule aliye mmiliki kabla na maingiliano yao yakiwa hayana tofauti sana,kwa vile muajiri mpya alikuwa akimkamuwa na kumnyonya kwa kumkodishakiwanja, nyumba, kumkopesha kwa matumizi ya chakula na mengineyo nakumlipisha riba ya kiwango atakacho bwanyenye. Ingawaje sio waajiri wotewaliyokuwa na mtindo huo , na inasemekana, hadhi ya watumwa Zanzibar ilikuwabora zaidi kuliko kwingi kwengineko, kwa sababu ya imani ya kiislam. Ubwanyenye ulikuwa njia ya uzalishaji mali bora zaidi ya uzalishaji mali wakiutumwa kwa vile ulipiga khatua kubwa zaidi katika kuendeleza uchumi hasa wakilimo, kuruhusu na kushajiisha kuweko kwa muuzaji wa bidhaa kama ni kiungobaina mali fulani na mali nyengine na hatimae mchuuzi huyu kuweza kuhodhi nakutajirika kwa kutosha na kuweza kutanua njia za usafiri na kuanzisha utumizi wa vifaa na mashine katika uzalishaji mali, kama vile meli za stima. Hatimae kuletauwezekano wa maendeleo ya mafundi, wahunzi na wengineo. Kufuatia njia yauzalishaji mali wa Kibwanyenye, pakazaliwa daraja jingine la uzalishaji malilijulikanavyo kama uzalishaji mali wa Kibepari, kama litavy okaririwa baadae, hiini njia muhimu ya uzalishaji mali ya wakoloni.
Utumwa na Uislaam
Wakoloni wote pamoja na wa kiingereza walifanya/na wamo wakifanya njama za siri za kujifanya wao wazuri na kuja kwao Bara la Afrika kulikuwa na madhumuni yakuleta kheri na fanaka pasi na kuwa na lengo jengine lolote, la siri au la dhahiri.Njia yao moja wapo muhimu waliyoitumia ilikuwa ni Makanisa na Mapadri. Kupigavita "ushenzi", "utamaduni uliyoselelea wa Kiafrika" na kuleta ustaarabu waKizungu lilikuwa ni jambo mojawapo waliyodai na kuliweka mbele. Tukifuata utamaduni wao tutakuwa kama wao kuvaa nguo zao, kula kama wao, kutumia vituvyao na kuuwauzia vitu kwa bei zao na kununua kutoka kwao, tukifanywa kuwana thamani kama zao. Wao, peke yao na wazungu wenzao, walidai kuwa walistaarabika, wengineo wote ni wakiwa hawajastaarabika na wakiwa washenzi,kwa mujib wa propaganda zao. Watu au tawala zozote zilizowaunga mkono Wangereza katika njama zao za kuwatawalia watu wengine walipewa heshima, ulwana ulinzi maalum. Kwa Zanzibar, wakoloni wa Kiingereza, baada ya kuwanyanganya khatamu zenyewe, ndio waliyoulinda na kuuhifadhi ufalme wa Kibunsaidi, lakini baadala yakuuita utawala huo kwa jina lililostahiki, yaani wa Kibunsaidi, walitunga mbinu zakuupa jina ambalo lili kuwa na azma ya kuwapa faida wao Wangereza zaidi. Kwahivyo wakaamuwa kuuita utawala huo ni wa Waarabu, na hata sio wa Kiomani auWakimanga, maana kwa kweli, sio Waarabu wa kila aina waliyotawala Zanzibar.Lengo la kuuita utawala huo ni wa Kiarabu, lilikusudia na shabaha nyenginekabisa, nalo ni kwamba Waarabu ni Waislaam. Kuuita utawala wa Zanzibar waKiarabu kulikuwa na shabaha mbili, moja wapo ni kuufanya Uislaama uonekanembaya na ukikandamiza Mwafrika na Uzungu na Ukiristo ukiwa ni mwema. Utumwa uli kuwepo Afrika ya Mashariki hata kabla ya kuzaliwa Nabii Issa, kwa hivyo kabla ya ufuasi wa Kiislaam wa Nabii Mohammad, salallah alayhi wasalaam. Lakini Mkolonikaufanya Utumwa umeletwa na Mwaarabu, wakati huo huo, kwa kweli, akikusidiakuchochea chini kwa chini na kusema ni Uislaaam ndio sababu ya Utumwa. Wakati ambapo utumwa ulipigwa marufuku Zanzibar, wakati huo huo, Wareno na Wafaransa walishughulika na biashara ya utumwa Afrika ya Mashariki, na kazihiyo waliifanya bila ya kuingiliwa kati na manuwari za Kiingereza zilizowekwamaalum kulinda usafirishaji wa watumwa. Mngereza, na vibaraka wake wakikiristo, hawasemi hayo wala hawasemi kwamba kulikuwa na Wangereza hapo hapo Zanzibar wakifaidika kutokana na jasho la Watumwa, na ndio maana mwanzoni kilekilichopigwa marufuku kilikuwa ni usafirishaji wa wa tumwa na sio kumilikiwatumwa. Walisahau vile vile kusema kwamba huko kwao hapo zamani kulikuwa nautumwa, ingawa huko makwao kulikuwa hakuna Uislaam. Wangereza walikuwahawat wambii juu ya maafa ya Waafrika wa Afrika ya Magharibi waliyopelekwa Marekani ya kaskazini kusini na Caribbean ambako hakukuwa na Uislaam. Wazunguwalipo kwenda Marekani walikwenda kwa niaba ya jina takatifu la Ukiristo, na kwa niaba ya jina la Msalaba, wakateteketeza wenyeji wa huko na kuwatawalia.
Njama za kuufanya Uislaam uonekane mbaya Afrika, ilikuwa kama kufanyakiini macho. Kuleta chuki za kugonganisha vichwa baina ya Wazanzibari kwa Wazanzibari, Watanganyika na Watanganyika, ili kuweza kuwatawala kwa urahisi na kuweza kutambaza dini ya ukiristo, hilo ndilo lilokuwa lengo muhimu la kampenihiyo, ingawa wengi wa wazungu hao walikuwa hata hawaamini Mungu, balikuutumilia ukiristo kuwatawalia na kuwanyonya Waafrika. Mkoloni alisahau kwambakwa niaba ya ukiristo Christofer Columbus aliwateketeza Wahindi Wekundu, nakazi hiyo ovu ikaja baadae ikaendelezwa na wenye asili ya Kiingereza na kufikahadi kwamba leo Wahindi Wekundu baada ya kuteketezwa wamekuwa wachache"minority" makwao wenyewe. Mkoloni hajatwambia kwamba huko Australia na NewZealand aliwateketeza wenyeji wa huko,"ma aborigens" kwa kutumia mbinu ovu mbali mbali, moja wapo ikiwa kuwagawiya watu wa huko mablangeti yaliyokuwa na magonjwa mbali mabli, kama vile tetekuwanga, kifua kikuu, ndui, magonjwa ambayo watu hao kwa wakati huo walikuwa hawana kinga viwili wilini mwao kuwezakujikinga na magonjwa hayo. Kwa vile watu hao siku hizo walikuwa hawakuchanjwawala kuwa na ulinzi wa kuzaliwa nao, walipukutika na kufiana kama nzige nahatimae Wangereza wakaweza kumiliki makoloni na kufanya sehemu hizo ni nchizao. Mitindo kama hiyo walikuwa wanataka kuifanya huko Afrika ya Kusini naZimbabwe, lakini wakaula na chuwa. Na sisi Wazanzibari, baadala ya kuamka nakuzitambuwa mbinu za Mkoloni za kutugonganisha vichwa, Waislaam kwa Waislaam,na Waafrika kwa Waafrika, tukabaki tunauwana wenyewe kwa wenyewe, baadalaya kukaa kitako na kujaribu kutatuwa tofauti zetu kwa njia za kisiasa na kidugu.Mkoloni alisahau kuwambia wananchi kwamba katika biashara ya utumwa Zanzibar ,kuwa Waislaam hawakufanywa watumwa na waliyosilim kutolewa utumwani.Lakusikitisha zaidi ni kuona hata wale waandishi na wataalam wanaosifika kuwawameendelea, wametekwa nyara na tafsiri ya ukoloni ya utumwa, na badala yakuukariri utawala huo kama ni wa kitabaka, mara nyingi na wao wan ajiingiza katikamtego wa kibaguzi. Hadi hii leo Uislaam unapigwa vita sana sehemu mbali mbaliulimwenguni, ingawa leo hazitumiwi sababu za utumwa bali sababu nyenginezo,kama vile kuvunja Katiba ya Muungano wakati Zanzibar ilipojiunga na Umoja wa Nchi za Kiislaam, na badala ya serikali ya Zanzibar kusimama kidete, kutetea utu, nchi na imani zao, ikakubali kamsujudia Nyerere. Kwa kutumia mbinu kama hizo, za kutumia Uislaam na Ukabila badala ya tafsiri yakitabaka, Mngereza alifanikiwa kuleta chuki na uhasama baina ya Wazanzibari,wakati yeye akishirikiana na kuuhifadhi utawala huo huo aliyouita wa Kiaarabu.Kwa njia kama hiyo Mngereza akafaulu kutufanya tukabane roho wenyewe kwawenyewe na kusahau kumpiga vita yule adui wa kweli, yaani Mkoloni wa Kiingereza. Hivi sasa Mngereza kesha ondoka hadharani, wamebaki vibaraka wakehasa huko Bara wanaoimba wimbo huo huo, ilhali babu zao (machifu) ndiowaliyokuwa wakikamata watumwa hao na kuwauza.
Ubepari
Ubepari nao ukifananishwa na Ubwanyenye, na Utumwa n.k. ni njia iliyoendelea bora zaidi katika kuleta maendeleo kwa jumla. Binaadam ni kiumbe anaeendelea kila usiku ukicha na siku zote atataka kuona anaendelea zaidi, kwa hivyo njiafulani ya maendeleo ikisha zorota inawekwa kando na kubadilishwa na njianyengine iliyo bora zaidi. Mngereza anadai kwamba aliuondosha utumwa Afrika ya Mashariki, lakini alisahau kusema, kama ilivyokaririwa hapo juu, kwamba kwao wenyewe waliendeleza uzalishaji mali wa utumwa na jamaa zao wa Marekani walijenga na kuendeleza njiaza uzalishaji mali wao kwa kupitia utumwa na hadi hii leo Waafrika wa Kimarekanibado wako katika daraja la chini kabisa katika jamii zote za huko Marekani.Kukomeshwa kwa utumwa Ulaya na Marekani kulipitishwa kwa sababu ya kwambaaina ya uzali shaji mali huo kwa wakati huo ulikuwa umesha zorota na haukuletafaida za kiuchumi tena. Mbali ya Mngereza kusahau kusema kwamba uchumi wasiku hizo ulikuwa haufaidiki tena kwa kutumia njia ya utumwa kwa vile amilikaewatumwa ilimbidi awalipie gharama zote za kila siku, gharama ambazo apata e uhuruwake ilimbidi ajihudumie mwenyewe. Vile vile amesau kusema kwamba vita vyakedhidi ya utumwa viliambatana na uenezaji wa utawala wake wa kikoloni na kusahaukusema kwamba uchumi wake ulifaidika kutokana na jasho la Watumwa.
Maendeleo ya uzalishaji mali ulimwenguni hayakwenda sambamba, kwa vile kuna nchi mbali mbali katika uliwengu wa tatu ambamo maendeleo ya uzalishaji malihayakufuata vidaraja kama vile vya nchi zilizoendelea, yaani kutoka utumwa, kwenda ubwanyenye halafu kwendea ubepari. Kutokana na upungufu wamaendeleo ya kisayansi na kiteknologia karibu nchi zote za ulimwengu wa tatu hadihivi leo hazijafikia kiwango cha uzalishaji mali wa kibepari. Mabepari wamehakikisha kwamba nchi hizi zinabaki nyuma na kuwa ni masoko ya bidhaa zamabepari ambao walikuwa ni wakoloni wao, na ardhi yao kuigeuza bustani za mauana mashamba ya chai, kahawa na viungo walivyovihitaji wao, wakati huo huo kuwani bidhaa zisoweza kushibisha walimao au kutoweza kuwahatarishiya uchumi wawakoloni. Ni hivi karibuni tu ambapo nchi chache za huko mashariki ya mbali ndizo zilizoruhusiwa kutumia uzalishaji mali wa kibepari. Hali hiyo imemkinika kwasababu ya gharama za uzalishaji mali huko Ulaya na Marekani zimekuw- a juu sanakutokana na kupigania haki za wafanya kazi huko nchi zilioendelea. Hali hii ikawafanya Mabepari wa nchi za magharibi kukimbilia zile nchi ambazo gharamahizo ziko chini na kujihakikishia na kuweza kuhakikisha faida kubwa zaidi. Kinyume na ilivyo dai la baadhi ya wataalamu fulani wa kisiasa na kihistoria, Zanzibar haikuwa na njia ya uzalishaji mali wa kibepari. Katika nchi zilizoendelea hasa zile za kibepari, uzalishaji mali wa utumwa kwa desturi hufuatiliwa na uzalishaji mali wa Kibwanyenye/Kimwinyi na hatimae ubepari kufuatia. Baada yakuondoshwa utumwa Zanzibar hapajatokea maendeleo yoyote ya maana ya uzalishajimali, bali msingi wa uchumi wa Zanzibar uliselelea pale pale na kuwa wa kale ukiwa wa Kibwanyenye na ukitegemea vuno la karafuu, nazi na pilipili hoho, napakitumika njia zile zile za kulimia za enzi za mababu na mababu. Ukulima wa vifaavya kisasa ulikuwa ni jambo duni, na viwanda vya aina yoyote, zaidi ya viwanda vya lazima vya ukamuaji wa mafuta ya karafuu na ya nazi, kiwanda cha sukari,kilicho-anzishwa na Barghash, vilikuwa duni. Uendelezaji wa uzalishaji maliulikuwa ni dufu, Zanzibar ikiwa shamba la kuchumiya ubepari wa kikoloni nakuselelea kuwa katika uzalishaji mali wa ki- bwanyenye na wakati huo huo, kupitia tabaka la Wafanya biashara, kuwa soko la bidhaa za kibepari kutoka kwa Wakoloni na kituo muhimu cha usambazaji wa bidhaa hizo katika sehemu nyengine za Afrikaya Mashariki na ya kati.
Ubwanyenye au Umwinyi ndio uliyokuwa mwenendo wa kitawala na wa kuzalisha mali Zanzibar na hadi leo hakuna mabadiliko makubwa katika fani hizi. Maingiliano . ya "kimwinyi na kiskwatta (squatter)" ndio maingiliano yaliyojenga msingi wakisiasa wa hivi sasa Zanzibar. Msingi huo ulionekana kama ni mfano wa kujengeamfumo wa uongozi wa vyama vya kisiasa viwili muhimu vya Zanzibar yaani ASP naZNP. Umwinyi au ubwanyenye vile vile ndio uliyokuwa msingi mmojawapo muhimuwa chuki za kikabila, hasa kwa vile ya mamwinyi au mabwanyenye wa Kizanzibariwalikuwa waliyokuwa na asili ama ya Kiarabu au ya Kishirazi na maskwatta wakiwawenye asili za Mrima/Bara. Misingi miwili mingine muhimu iliyoleta chuki baina yajamii ya Kizanzibari ilikuwa ni utawala wa Kisultan na utawala wa Kiingereza.Ingawaje, kabla ya kuja tawala mbili hizo Zanzibar, tawala za wajukuu wa Hassan,Sultan wa Shiraz, hasa ya utawala wa Mwinyi Mkuu, ilikuwa ni tawala iliyotumiautumwa kama ni njia ya uzalishaji mali - wa hapo kale. Zanzibar ilipokuja chini ya mamlaka ya Seyyid Said bin Sultan (1832) palikuwa na makubaliano baina ya Sultan huyo na Sultan Mwinyi Mkuu kwamba, kila mmoja atawale na kuwa na mamlaka ya sehemu yake, hatimae pakatokea mfarakano mkubwa kwa vile Seyyid Said alichukuwa utawala wote hata kutia ndani aukuhamisha nchi tawala za Kishirazi. Inasemekana kwamba, kabla ya utawala wa Mabusaidi kutawala Zanzibar,Wazanzibari walipeleka Ujumbe kwa Sultani wa Omani, wakiwaona kama Waislaam wenzao, waende Zanzibar kuwasaidia kuondowa utawala wa makafiri wa Kireno. Usultani huo hatimae ukaifanya Zanzibar mamlaka yake, pekee. Mabwanyenyewenye asili ya Kiomani wakawa hatimae ndio wenye kumiliki ardhi kwa wingi zaidi na kunufaika zaidi kiuchumi na hali hii ikawafanya kuwa tabaka la juu kabisa Zanzibar na wenyeji wao, Mabwanyenye wa Kishirazi, wakashushwa hadhi na kuwatabaka dhaifu zaidi. Ingawaje, hili ni tabaka lililojiwe za zaidi kuliko Waswahili wengine waliyokuwa hawana asili ya Kizanzibari halisi. Karibu wote hawa wa kundila mwisho walikuwa katika tabaka la chini. Utawala wa kisultani Zanzibar haukuwa wa Kiislaam, au wa Kiarabu kama Wangereza walivyotufanya tuamini, kwani watawala hao hawakutawala kwa mujib sheria za kiislaam na hawakutoka Arabuni kote bali walitoka Omani na hata huko Omani walikuwa ni watu wa ukoo mmoja tu, nao ni Mabusaidi na sio aina zote zaMabusaidi. Na hata wale mabwabyenye wengine wa Kiomani waliyokuwa matajiri,kuwa na mashamba na nguvu nyingi hawakuwa watu ambao wakiwakilisha maslahiya utawala wa Kibusaidi tu. Baadhi yao, kama vile ilivyo desturi katika baadhi yawatawala au mabwanyenye tofauti, kulikuwa na migongano, michuano na mivutanoya kujinufaisha binafsi. Katika Zanzibar, kwa mfano, wengi wa Mabarwani hadi siku za mwisho za Usultani walisemekana kuwa wakipinga Ufalme na msimamo huo walikuwa nao tokea siku za Juma Barwani alipochukuwa silaha kupambana na Seyyid Said bin Sultan.
0 comentários:
አስተያየት ይለጥፉ