DAR ES SALAAM - TANZANIA

 

Dar es Salaam

Dar es Salaam ni jiji kubwa kuliko yote nchini Tanzania. Pia ni jina la Mkoa wa Dar es Salaam.

Ni mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania wakati Dodoma ni makao makuu ya Tanzania tangu mwaka 1973. Mpango wa kuhamishia serikali mjini Dodoma bado unaendelea, japokuwa bado ofisi nyingi za serikali, ikiwa ni pamoja na Ikulu, zipo Dar es Saalaam.

Mji una wakazi wapatao 4,364,541 kwa hesabu ya sensa iliyofanyika katika mwaka wa 2012.

Jiji hili zamani liliitwa Mzizima. Sultani Seyyid Majid wa Zanzibar ndiye aliyelipa jiji hili jina "Dar es Salaam" linalotokana na lugha ya Kiarabu دار السلام (Dār as-Salām) lenye kumaanisha "nyumba ya amani." Maelezo yanayopatikana mara nyingi kuwa maana ni "bandari ya salama" yachanganya maneno mawili yanayofanana katika Kiarabu yaani "dar" (=nyumba) na "bandar" (=bandari).

Dar es Salaam ilichaguliwa na wakoloni Wajerumani kuwa mji mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa sababu ya bandari asilia yenye mdomo mpana wa mto Kurasini. Hivyo kuanzia mwaka 1891 Dar es Salaam ilichukua nafasi ya Bagamoyo kama makao makuu ya utawala.

Bandari pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwenda Kigoma tangu mwaka 1904 viliimarisha nafasi ya mji ulioendelea kama mji mkuu baada ya Tanzania bara ya leo kuwa eneo lindwa la Tanganyika chini ya Uingereza.

አንተ ይፈልጋሉ? አጋራ:

ተዛማጅ ልጥፎች